Naambiwa Mzee Edward Lowassa mwamba wa siasa za Tanzania amerejea CCM.
Huu ni ushindi mkubwa kwa Lowassa mwenyewe na vyama vya Upinzani.
Lowassa atapata posho zake za uwaziri mkuu bila mizengwe.
Lowassa kwa umri wake na hadhi yake si mtu wa kushinda mahakamani au gerezani kwa mapambano ya kidemokrasia.
Mkwe wake Sioi Sumari kama sijajosea jina yupo ndani kwa kosa la uhujumu uchumi tangu 2016.
Kwa kipindi chote hicho,binti wa Lowassa anaishi kama mjane kwa kumkosa mume wake,
Kurejea kwa Lowassa CCM ni fursa kwa mwanae kumpata mume wake mapema ndani ya miezi mitatu ya mwanzo.
Hivi mlitaka Lowasa abaki upinzani huku akijua chaguo la Upinzani ni Lissu au Zitto halafu abaki huko kwa faida gani wakati mkwe wake anateseka gerezani?
Mzee Lowassa kajitendea haki yeye,familia yake pamoja na mkwe wake.
Mzee kaamua kuzichanga na kubani kuwa kurudi CCM kuna faida nyingi kuliko kubaki upinzani ambako si chaguo lao tena kwenye uchaguzi mgumu saana wa 2020.
Kwa upande wa upinzani nako ni sherehe.
Kuondoka kwa Lowassa kumetoa fursa kwa upinzani kujipanga mapema.
Upinzani ungeumizwa endapo Lowassa angejiondoa Upinzani katikati ya kampeni za mwaka 2020.
Kuondoka kwa Lowassa kwa hiyari yake kumeunusuru upinzani na Migogoro ya ndani ambayo kwa sasa ipo ndani ya CCM kuliko upinzani.
Kama wangemuengua Lowassa kwa nguvu na yeye kuamua kuwavuruga kama anavyofanya Lipumba,hakika upinzani ingebidi usubiri hadi 2025.
Lakini kwa kitendo cha kiungwana alichofanya Mzee Lowassa kutotaka usumbufu na kuvunjiwa heshima,ameamua kujiondoa mwenyewe .
Kurejea kwa Lowassa CCM ni sawa na kuamua kustaafu siasa akiwa ndani ya chama kilichomlea. Hii ni faida kwake binafsi kwakuwa ataendelea kunufaika na mfumo ikiwa CCM itadumu nadarakani.
Familia yake haitataifishwa mali zao hata siku Lowassa akiaga Dunia siku mwenyezi mungu akimuita.
Vijana wa upinzani sitegemei mumtukane ,kumzodoa na kumkejeli Mzee wetu huyu ambae ameusaidia upinzani kupata viti vingi bungeni kutokana na ushawishi wake.
Siasa ni wakati,Mzee amesoma vizuri alama za nyakati.
Siasa ni wakati, Mzee LOWASSA Amesoma Vizuri Alama za nyakati
0
March 02, 2019
Tags