Simba SC, Yaendeleza Uteja Mechi za ugenini Ligi ya Mabingwa


Bingwa mtetezi wa Ligi kuu Tanzania bara, Simba SC,  imeendeleza rekodi ya kupoteza mechi za ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya usiku huu kuchapwa mabao 2-0 na wenyeji, JS Saoura Uwanja wa Agosti 20, 1955 mjini Bechar katika Kundi D.

Katika mchezo huo Simba ilianza kufungwa katika kipindi cha kwaza dakika ya 18 gori lililofungwa na mshambuliaji Sid Ali Yahia Cherif kwa shuti kali akimalizia mpira uliorudi baada ya kuokolewa na Paul Bukaba kufuatia yeye mwenyewe kuunganisha kwa kichwa krosi ya Mohamed El Amine Tiboutine kutoka upande wa kulia.

Akafuatia Mohamed El Amine Hammia kufunga bao la pili kwa penalti dakika ya 51 baada ya Sid Ali Yahia Cherif kuangushwa na beki wa Simba SC, Paul Bukaba Bundala kwenye boksi.

Kwa matokeo hayo, Saoura inapanda kileleni mwa Kundi D ikifikisha alam nane baada ya kucheza mechi tano, ikifuatiwa na Al Ahly, AS Vita zenye pointi saba kila moja, huku Simba SC  ikishika mkia katika Kundi D kwa pointi zake sita, huku ikiwa ndio timu iliyofungwa mechi nyingi hadi sasa katika kundi lao.

Mechi za mwisho Machi 16, Al Ahly na JS Saoura nchini Misri na Simba SC na AS Vita mjini Dar es Salaam zitaamua timu za kwendsa Robo Fainali kutoka Kundi D.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad