Simba Yapiga Hesabu Kali... Yajipanga Kuchukua Pointi 3 kwa JS Saoura

Simba  Yapiga Hesabu Kali... Yajipanga Kuchukua Pointi 3 kwa JS Saoura
UONGOZI wa Simba umesema kuwa hesabu kubwa leo ni kuona wanapata pointi mbele ya wapinzani wao JS Saoura kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa utakaochezwa nchini Algeria.

Simba wana kibarua kizito leo kutokana na kuwa na matokeo mabaya ugenini hasa baada ya kutinga hatua ya makundi kwani kwenye mechi mbili ambazo walitoka zote walifungwa, walianza mbele ya AS Vita wakafungwa 5-0 kisha mbele ya Al Ahly walipigwa 5-0.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema wanatambua ugumu wa mechi ila watapambana kupata matokeo.

"Ni mchezo mgumu na wenye ushindani ila hesabu kubwa ni kuona tunapata matokeo ili tuweze kusonga mbele kwani kila mmoja anahitaji kwenda hatua ya robo fainali, mashabiki msisahau kutuombea," amesema Manara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad