Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Nyakoro Sirro, amewaomba viongozi wa dini pamoja na wale wa siasa kulisaidia jeshi la polisi kupaza sauti na kutoa elimu juu ya mambo ya ubakaji jambo ambalo
Akizungumza leo na wanahabari, Jijini Dar es salaam, Kamanda Sirro amesema matukio ya kubaka yamekuwa changamoto kubwa kuliko uhalifu wa uporaji na matukio mengine.
Sirro amesema matukio ya ubakaji yameenea kwa kasi kutokana na mmomonyoko wa maadili.
Ameeleza kwamba wapo wanaume wenye umwri mkubwa lakini bado wanaenda kimapenzi na watoto wenye umri chini ya miaka 18 pasipo kujua kwamba hata kama ameridhia, "bado kisheria atakuwa anabaka".
Sirro amesema kwamba kama jeshi la polisi kwa sasa linajipanga kuhakikisha kwamba wanatoa elimu mashuleni ili kuweza kuwajengea uelewa wanafunzi waweze kuepuka ulaghai.