Sumaye Afunguka Kinachowafanya Watu Waondoke CHADEMA Na Kurudi CCM

Sumaye Afunguka Kinachowafanya Watu Waondoke CHADEMA Na Kurudi CCM
Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani CHADEMA Fredrick Sumaye, amesema yapo mashinikizo mbalimbali yanayowataka viongozi waliotoka Chama Cha Mapinduzi na kuhamia Upinzani warudi ndani ya Chama hicho huku akibainisha kuwa vitendo vingine wanavyofanyiwa ni vya kuwaumiza.

Akizungumza na kipindi cha East Africa Breakfast kinachoruka East Africa Radio, Sumaye amesema wapo watu wanaowafuata na kuleta maneno, na hata kutendewa mambo mbalimbali ya lakini yeye bado ameendelea kuwa na msimamo wake.

Amesema kwamba wakati anahamia CHADEMA alikuwa na maamuzi yake hiyo hawezi kujali vitendo anavyofanyiwa au kwa kushurutishwa na mtu.

"Mimi nilipotoka CCM nilitoka kwa hiyari yangu. Siwezi kurudi kwa kushurutishwa na mtu yeyote. Siyo maneno tu yanayotutaka turudi huko, bali yapo mambo mengi tunatendewa ili turudi lakini kila mtu ana uamuzi wake. Kama una maamuzi yako imara hata kama utatendewa mambo fulani fulani utasimama na misimamo yako huku unaumia", ameema Sumaye.

Akizungumzia kuhusu madhara na aathari ambazo Lowassa atazisababisha kwa kuhama Chama, Sumaye amesema CHADEMA ilikuwa imara hata kabla ya Lowassa kujiunga nao.

"Lowassa alikwenda CHADEMA baada ya kuonekana kwamba ameonewa kule CCM, lakini siyo kwamba tulikikuta sifuri. Tulikuta chama hiki kimeshajiimarisha sehemu nyingi hata kama siyo nchi nzima lakini kilishakuwa kikubwa.

"Tuseme ukweli yale mafuriko ya 2015 hayakusababishwa na Lowassa pekee kwani hata 2010 wakati Dk. Slaa anagombea na Kikwete utaona tofauti ilikuwa ndogo ni kwamba watu wanataka mabadiliko," Sumaye.

Sumaye ameongeza kwamba, "Kuna factor ya kwamba watu walishaichoka CCM tangu 2010 wakataka mabadiliko lakini hata sasa watataka mabadiliko sana, kuondoka kwa Lowassa hakuwezi kusababisha pengo".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad