"Tembeeni Kifua Mbele" - Rais Magufuli

"Tembeeni Kifua Mbele" - Rais Magufuli
Rais wa Rwanda Paul Kagame leo 08 Machi, 2019 amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 2 hapa nchini na kurejea nchini kwake, ambapo hapo jana alifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Mara baada ya kuagana na mgeni wake Rais Magufuli amesalimiana na wananchi wa Dar es Salaam waliojitokeza kumuaga Rais Kagame ambao wengi wao walikuwa ni wanawake na kuwatakia heri ya Siku ya Wanawake Duniani.

Rais Magufuli amewashukuru wanawake wote kwa mchango mkubwa kwa taifa na amesema serikali inatambua na kuthamini juhudi zao mbalimbali.

“Mungu awabariki sana akina mama, mnafanya kazi nzuri kwa ajili ya taifa hili, endeleeni kuimarisha umoja wa Watanzania wote, serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri zinazofanywa na akina mama, endeleeni kutembea kifua mbele, Mungu atawalinda, na mimi sasa hivi naondoka kwenda kumuona mama yangu hospitalini katika siku yake hii, pia natoa shukrani nyingi kwenu na kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya kwa jinsi mnavyojitolea kuwapokea na kuwaaga vizuri wageni wetu”, ameongeza Rais Magufuli.

Rais wa Rwanda Paul Kagame Paul Kagame aliwasili jana ambapo alipokelewa na viongozi mbalimbali wa  Mkoa wakiwemo Wakuu wa Wilaya wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad