Tetemeko la ardhi lililodumu kwa takriban dakika moja leo mchana Alhamisi Machi 21, 2019 limetokea mkoani Mbeya na kuzua taharuki huku baadhi ya wananchi na wafanyakazi katika ofisi mbalimbali wakitimua mbio.
Baadhi walilazimika kuacha ofisi zao huku waliopo nyumbani nao wakitoka nje ya nyumba zao, hata hivyo hakuna madhara yaliyoripotiwa hadi sasa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Earthquake Track kumetokea tetemeko la ardhi lenye ukubwa (magnitude) 5.1 mjini Sumbawanga. Baadhi ya wakazi wa mkoani Mbeya pia wameripoti kutokea kwa tetemeko la ardhi mkoani humo
Tetemeko la Ardhi Latokea Mbeya na Kuleta Taharuki Kubwa
0
March 21, 2019
Tags