Trump afunguka haya kuhusu Kim


Licha ya mkutano wa kilele kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kuvunjika Trump amesema kuwa uhusiano wake na kiongozi huyo ni mzuri.

Trump aliandika katika mtandao wake wa Twitter siku moja baada ya kurejea Washington na kusema kuwa mazungumzo kati yao yalikuwa ya msingi.

Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba mazungumzo yao yalivunjika kwa sababu Kim alisisitiza kwamba vikwazo vyote dhidi ya Korea Kaskazini vinapaswa kuondolewa, bila ya nchi hiyo kuachana na mpango wake wa nyuklia.

Ameongeza kusema kuwa Marekani inajua Korea Kaskazini inataka nini na nchi hiyo pia inajua kile ambacho Marekani inapaswa kuwa nacho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad