Hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kuhama chama chake cha muda mrefu na kuhamia ACT - Wazalendo, imeonekana kumuweka kwenye wakati mgumu mbunge Ally Saleh ambaye ni miongoni wafuasi wake.
www.eatv.tv ilimtafuta Mbunge huyo wa Malindi Visiwani Zanzibar, ambaye ni miongoni mwa wabunge ambao walikuwa upande wa Maalim ili kufahamu msimamo wao baada ya Maalim Seif kuhama chama.
"Mimi siwezi kuongea chochote kwa sasa, nitaweza kuzungumzia suala hilo baada ya siku 2" amesema Mbunge wa Malindi Ally Saleh.
Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.
Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama majira ya saa nane leo Machi 18, 2019, alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.
TOP STORIES
SPORT
“Shughuli ya Lechantre imekwisha”-Manara
SPORT
Ngoma ashindwa kuichezea Azam, Kagame
CURRENT AFFAIRS
Amuua mke mwenza na kumzika shambani
CURRENT AFFAIRS
Mbunge wa CHADEMA, ajiuzulu na kujiunga CCM
MOST POPULAR
ENTERTAINMENT
Amber Ruty acheza utupu jukwaani
SPORT
Simba kupeleka timu nne michuano ya vilabu Afrika
CURRENT AFFAIRS
Katibu Mkuu CHADEMA atoa neno kuhusu Maalim Seif
SPORT
Baada ya Simba kufuzu, Manara atatimiza ahadi?
CURRENT AFFAIRS
Makamu wa Rais atangaza ajira 500
ABOUT US
ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS
NETWORK
IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO
© 2019 East Africa Television Limited. All Rights Reserved