Uganda waanza na wachezaji 46, Okwi baadaye

Kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Sébastien Desabre ametaja majina ya wachezaji 46 wa timu ya taifa, kwaajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wa mwisho wa Kundi L kuwania kufuzu AFCON 2019.


Desabre  ambaye timu yake tayari imeshafuzu fainali hizo zitakazofanyika Misri, amesema watakaoripoti kwasasa ni wachezaji 31 ambao baadaye watachujwa na kusalia tisa ambao wataungana na wachezaji wengine 15 wanaocheza nje ya ya Uganda.

Aidha Desabre amesema baada ya kuita wachezaji wa nje ya Uganda wakiwemo Emmanuel Okwi, Juuko Murshid wote wa Simba, watakuwa 24 na wataingia kwenye kambi ya muda mfupi itakayokuwa nchini Misri kuanzia Machi 18 hadi 22.

Uganda watacheza dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa Machi 24 mchezo ambao ni wa mwisho kwenye Kundi L na utaamua timu gani inaungana na Uganda kwaajili ya fainali hizo.

Tanzania ipo Kundi L na timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho.  Uganda wanaongoza kundi na pointi 13, wakifuatiwa na Lesotho wenye pointi 5 sawa na Tanzania iliyopo nafasi ya tatu na Cape Verde anashika mkia na alama 4.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad