Ukawa watajwa kuwa hoi

Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman Khalifa, amesema wao kama chama cha Wananchi wameshajitoa kwenye mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi 'UKAWA' kwa madai upo hoi na hauna msaada kwao.


Khalifa amesema kwamba, msimamo wa CUF ni kutoshirikiana na UKAWA kwa sababu wabunge wa CHADEMA na wafuasi wake wameshindwa kuwa na ushirikiano katika matatizo waliyokuwa nayo.

Akizungumza na www.eatv.tv Khalifa amesema kwamba huo Umoja wa Katiba ya Wananchi kwa upande wao wanaona kama haupo, hivyo wao wameshajitoa huko.

"Ukawa wenyewe  upo hoi bin taabani. Haupo mimi sidhani kama upo" amesema.

Ameongeza kwamba kwa muda mrefu Wabunge wa CHADEMA wamekuwa wasemaji wa wabunge waliokuwa wakimuunga mkono, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif ambaye kwa sasa amehamia chama cha ACT Wazalendo.

"Wabunge wa CHADEMA walikuwa wazungumzaji wa wabunge wa CUF ya Maalim Seif. Sisi tunakwenda mahakamani watu wa CHADEMA wanakuja kutufanyia fujo, ilikuwa ina wahusu nini wakati yale yalikuwa matatizo ya ndani ya chama. Sisi tumeshasema hatuwezi kufanya kazi na UKAWA badala ya kushirikiana kisiasa na kibinaadam, unakuwa ni ushirikiano wa kiadui na kupandikizana chuki".

Umoja wa Katiba ya Wananchi, (UKAWA) uliundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, NLD, CUF na CHADEMA ambapo baadaye waliungana katika uchaguzi mkuu wa 2015 na kusimamisha mgombea mmoja wa Urais ambaye alikuwa Edward Lowassa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad