Umoja wa Madereva wa serikali watoa tamko

Umoja wa Madereva wa serikali watoa tamko
Uongozi wa Chama cha Madereva wa Serikali mkoani Kigoma umeomba uboreshwaji mazingira ya kazi kwa madereva wa umma kutokana na baadhi yao kulalamikia kutokulipwa kwa wakati na kufanya kazi hiyo bila mikataba.

Akielezea changamoto za kiutendaji kwa madereva wa magari ya umma, Mwenyekiti wa Madereva wa Serikali kitaifa, Richard Peter amebainisha kuwa baadhi ya madereva wanafanya kazi katika mazingira magumu na bila kutambulika kisheria hivyo ameiomba wizara husika kusaidia utatuzi wa jambo hilo.

"Madereva hawana hata taarifa zozote zinazowatambulisha katika kazi yao, unakuta gari lina thamani ya sh. milioni 100 au 200 lakini dereva anayeiendesha hiyo gari hana hata 'Written Document'. Mfano hapa Kigoma wanalipwa kwa hisani, unaweza kumkuta mtu anakwambia nina miezi mitatu nimelipwa elfu 30", amesema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Kigoma, Aziz Mtambuzi akiongea na viongozi wa madereva hao na madereva kutoka halmashauri za wilaya za Kibondo, Uvinza, Kasulu na Kankonko amesema wao kama serikali wanaendelea kuboresha na kutatua changamoto huku akiwataka kufanya kazi vizuri na kutunza magari ya umma ili kuipunguzia serikali gharama za matengenezo.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad