Umoja wa Mataifa Waanza Kuondoa Wanajeshi wa Kulinda Amani DRC

Umoja wa Mataifa Waanza Kuondoa Wanajeshi wa Kulinda Amani DRC
Umoja wa Mataifa 'UN' umeanza kuweka mipango ya kuanza kuwaondoa wanajeshi wa kulinda amani kutoka katika Nchi ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa ni kubadilisha malengo ya jeshi hilo nchini humo.

Hatua hii imebainishwa na Afisa wa Umoja wa Mataifa, amesema baada ya kuona hali ya kiusalama kuanza kuimarika katika maeneo kadhaa, na hali ya kisiasa kubadilika na nchi hiyo kuwa na Rais mpya.

Jeshi la Umoja wa Mataifa limekuwa nchini DRC kwa karibu miaka 20, likiwa na wanajeshi wapatao 16,000 lengo likiwa ni kuwalinda raia na kuzuia mashambulizi ya waasi, lakini raia wengi wa DRC hasa kutoka Mashariki mwa nchi hiyo wamekuwa wakisema kwa kiasi kikubwa jeshi hilo halijasaidia.

Iwapo mpango huo utafanikiwa, huenda katika siku zijazo idadi ya wanajeshi wa MONUSCO itaanza kupunguzwa na hili linakuja wakati huu muda wa kuhudumu kwa jeshi hilo ukitarajia kumalizika kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa ni lazima MONUSCO ishirikiane kikamilifu na serikali ya rais Felix Thisekedi kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo yanafanyika na kurejesha amani ya kudumu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad