Mipango ya kuwatenga wanariadha wa kike kulingana na viwango vyao homoni za testosterone “Ni ukiukaji wa haki Kimataifa za biadamu ” linasema Baraza la haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.
Mshindi wa mbio za Olympic mita 800 Caster Semenya, mwenye umri wa miaka 28, anapinga nia ya Shirikisho la kimataifa la Riadha (IAAF) juu ya mpango kuweka masharti ya viwango vya testosterone miongoni mwa wanariadha wa kike.
Umoja wa mataifa imeitaja mipango hiyo kama “isiyo na umuhimu , ya udhalilishajia na yenye mathara “. IAAF imesema kuwa muswada uliopatiwa Umoja wa Mataifa unajumuisha “kauli zisizo sahihi”.
Umoja wa Mataifa wazitaka bodi za michezo kuacha kuandaa na kutekeleza sera zinazowasukuma wanariadha wanawake na wasichana kupitia tiba zisizo za lazima
Chini ya sheria za IAAF, mwanariadha wa kike mwenye viwango asilia vya juu vya homoni za testosterone anatakiwa kukimbia na wanaume au kushiriki mashindano ya watu waliobadilishwa mpaka apate tiba ya kupunguza viwango hivyo.
Sheria hizo zinawahusu wanawake wanaokimbia mbio za mita 400 na maili moja na inawapasa wanariadha hao kuhakikisha viwango vya testosterone vinakuwa chini kulingana na kiwango kilichowekwa. “kwa walau miezi sita kabla ya mashindano “.
Suala hilo lilijadiliwa na kikao cha 40 cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa cha mwezi Machi, ambapo wajumbe waliomba ripoti yenye maelezo ya kina juu ya suala hilo iandaliwe kwa ajili ya mkutano ujao.
Kabla ya hayo, baraza hilo lilielezea “hofu zake ” juu ya mapendekezo ya IAAF. Baraza hilo limesema bodi za utawala hazinabudi “kuacha kuandaa na kutekeleza sera na utendaji ambao unalazimisha , kushurutisha au kuwasukuma wanariadha wanawake na wasichana kupitia , udhalilishaji na mathara ya upasuaji wenye madhara wa kimatibabu usio wa lazima kama njia ya kuruhusiwa kushiriki katika matukio mashindano ya michezo ya wanawake”.
Katika taarifa yao iliyochapishwa katika jarida la matibabu la Uingereza, hivi karibuni wataalamu walidai kuwa sheria za IAAF zinaitia katika hatari ya “kuweka viwango visivyo vya kisayansi kwa matukio mengine ya faida za maumbile “.
IAAF ilitaka kuweka sheria mpya tarehe 1 Novemba 2018, lakini ikakabiliwa upinzani wa kisheria uliolazimisha kusheleweshwa kwa utekelezwaji wake hadi Mahakama ya utatuzi wa migogoro ya michezo (Cas) itakapoamua juu ya suala hilo.
Wanariadha wa kike kama Caster Semenya wanatakiwa kukimbia na wanaume kulinga na sheria za IAAF
Chini ya sheria za IAAF, mwanariadha wa kike mwenye viwango asilia vya juu vya homoni za testosterone
Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa tarehe 26 Machi, lakini Cas iliiahirishahadi mwezi ujao.
Ushindi kwa Semenya utamfanya awe huru kuendelea kushiriki mashindano kama ambavyo amekuwa akifanya, lakini iwapo atashindwa kwenye kesi hiyo itamaanisha kuwa mwanariadha huyo wa Afrika Kusini anaweza kutoshiki mashindano, kushindana na wanaume au kulazimika kutumia dawa za kushusha viwango vyake vya homoni
Awali Semenya aliagizwa na wakuu wa riadha afanyiwe vipimo vya jinsia, lakini hakuna matokeo ya vipimo hivyo yaliyotangazwa rasmi kwa umma.
Testosterone ni homoni inayoongeza ukubwa wa misuli, nguvu za mwili na chembechembe nyekundu za damu,ambayo hathiri uwezo wa nguvu za mwili.
Katika taarifa iliyotolewa kwa BBC kitengo cha Spoti IAAF ilisema “ni wazi kwamba mwandishi wa ripoti hakuwahi kuona maelezo ya sheria za IAAF wala maelezo taliyowasilishwa hivi karibuni katika Mahakama ya utatuzi wa migogoro ya michezo.
” Kuna kauli ambazo si sahihi zilizomo kwenye muswada uliowasilishwa katika baraza la Haki za binadamu la umoja wa Mataifa kwa hiyo ni vigumu kujua ni wapi pa kuanzia.
” Tunalokubaliano sote ni kwamba tunaamini ni muhimu kuzingatia usawa katika mashinda ya michezo ya wanawake ili wanawake wawe huru kushiriki katika mashindano ya kitafa na kimataifa ya michezo .
” Kufanya hili ni muhimu ili kuhakikisha mashindano yaliyotengwa kwa ajili ya wanawake yanalindwa, jambo linalohitaji shertia na masharti ili kulilinda, vinginevyo tunajiweka katika hatari ya kupoteza kizazi kijacho cha wanariadha wanawake, kwani hawataona njia ya mafanikio katika michezo ya kike.”
Umoja wa mataifa waingilia sakata la IAAF kutaka kumtenga mwanariadha Caster Semanya kuhusu jinsia yake
0
March 26, 2019
Tags