Utafiti: Watumiaji wa Simu za Tekno Huweka Nyimbo za Kawaida Kama Miito ya Simu zao


Kawaida ya hoja hujibiwa kwa hoja, utafiti hupingwa kwa utafiti.

Iko hiviii wale ndugu zangu wanaomiliki au kutumia simu zinazotengenezwa na kampuni ya Tekno ndio hupendelea kutumia nyimbo za kawaida (muziki) kama miito ya simu zao, nyimbo za bongo fleva, reggae, nyimbo za kiingereza iwe rap n.k, wanabadilisha mara kwa mara leo harmonize, kesho sijui Harmorapa, mara Beyonce n.k

Hii ni tofauti sana na watumiaji wa brands zingine kama Iphone, Samsung, Oppo , Xiaomi na wengineo. Watumiaji wa kampuni hizi zingine hutumia mtetemo(vibrations) na ringtones zinazokuja na simu moja kwa moja.

Kwa udadisi wangu nimebaini watu hawa hufanya hivyo ili kuvuta attention ya watu wengine ili ionekane na wao wanamiliki simu janja (smartphone).
Wengine ni wale wanaotoka up country hivyo wakiingia mjini hutaka kila mtu ajue kwamba na wao wamenunua au wanamiliki simu janja.

Tabia ya watu hawa hufanana na watumiaji wa infinix phones usibishe fuatilia tu

Good morning all
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad