Video Milioni 1.5 za Shambulizi la New Zealand zaondoshwa mtandaoni na Facebook


Mtandao wa kijamii wa Facebook umeondoa picha za video Milioni 1.5 kuhusu shambulizi la misikiti katika mji wa Christchurch nchini New Zealand, saa 24 baada ya kutokea kwa shambulizi hilo.

Mkuu wa Facebook nchini New Zealand, Mia Garlick amendika kwenye ukurasa wa twitter kwamba wataendelea kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji wa kimaudhui kwa kutumia teknolojia pamoja na watu.

Amesema wanaondoa pia video zilizofanyiwa marekebisho ambazo hazionyeshi picha ya tukio hilo, kwa heshima ya wale walioathiriwa na shambulizi hilo na wasiwasi ulioonyeshwa na mamlaka za nchini humo.

Muda mfupi baada ya shambulizi, polisi ilisema inalishughulikia suala hilo, huku ikiwataka watu kutozisambaza zaidi vidio hizo, matamshi yaliyorudiwa na waziri mkuu wa New Zealand, Jacinda Arden.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad