Dkt. Mahenge ameyasema hayo katika ziara yake ya siku moja ya ukaguzi wa miundombinu mbali mbali ikiwemo, barabara katika eneo hilo pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Miyuji jijini Dodoma.
Naye Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin kunambi aliyeambatana na mkuu wa mkoa katika ziara hiyo amesema kuwa eneo hilo lina viwanja vipatavyo elfu kumi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobasi Katambi amesema, serikali imekwishawalipa fidia wananchi waliyokuwa wakilalalimikia maeneo yao kutwaliwa.
Kufuatia ziara hiyo wananchi wa ndani na nje ya Dodoma wamehaswa kutovamia maeneo na kutonunua viwanja kiholela bali wafate taratibu za ununuzi wa viwanja vinavyouzwa na Halmashauri ya Jiji hilo jambo litakalofanya kuepusha migogoro ya ardhi katika Jiji hilo