Wachezaji wa Simba Watoa Ahadi

Wachezaji wa Simba Watoa Ahadi
Nahodha wa Simba John Bocco ameahidi kuwa wachezaji wote wapo kwenye morali nzuri ya mchezo na wapo tayari kuandika historia nyingine kwa klabu na Tanzania kwa ujumla.


Akiongea kwenye mkutano kabla ya mechi (Pre-Match meeting), Bocco amesema wamefanya mazoezi kwa siku mbili tangu watoke Algeria na wako vizuri kwa ajili ya kutafuta ushindi.

''Tunaiheshimu AS Vita ni klabu yenye uzoefu katika michuano hii, lakini na sisi kama Simba ni klabu kubwa na tumejiandaa, tunataka kuweka historia jambo ambalo linawezekana.

Mbali na hilo Bocco amaewaomba mashabiki waje uwanjani kwa wingi kuishangilia Simba kwani kwa kufanya hivyo watawapa nguvu zaidi nje ya uwanja na hatimaye kufanikiwa kushinda.

Simba inahitaji ushindi pekee leo ili iweze kusonga mbele kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutoka Kundi D, lenye timu za Al Ahly, AS Vita na JS Saoura.

Al Ahly pia leo wanakuwa wenyeji wa JS Saoura huko Misri mchezo ambao utapigwa muda mmoja na wa Simba ambao ni saa 1:00 usiku.

Msimamo wa Kundi D

JS Saoura pointi 8
Al Ahly pointi 7
AS Vita poini 7
Simba SC pointi 6
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad