Wafanyakazi 22 wa UN wafariki katika ndege ya Ethiopia

Wafanyakazi 22 wa UN wafariki katika ndege ya Ethiopia
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) limetoa pole kwa nchi, familia na ndugu waliopoteza jamaa zao 157 kwenye ajali ya ndege ya Shirika la Ethiopia iliyotokea jana Jumapili na kubainisha kuwa walikuwamo wafanyakazi wake 22.

Shirika hilo limetoa taarifa Leo Machi 11 imeeleza kuwa wafanyakazi hao kutoka maeneo tofauti duniani walikuwa wanakuja Nairobi kuhudhuria mkutano wa Shirika la Mazingira (UNEA).

Akisoma taarifa hiyo katika kikao cha dharura cha zaidi ya wajumbe 4,700 wanaohudhuria mkutano huo, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Habitat), Maimunah Sharif amesema UN inaungana na familia pamoja na nchi zilizopoteza jamaa zao kuomboleza vifo hivyo.

"Tumepoteza wafanyakazi 22. Ni pigo kubwa kwetu Walikuwa wanakuja kuungana nasi hapa. Umoja wa Mataifa unatoa pole kwa familia na ndugu waliopoteza wapendwa wao," amesema Maimunah.

Waalikwa wanaohudhuria mkutano huo walisimama kwa dakika moja kutoa heshima kwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo, asubuhi ya leo baada ya kuthibitika kwa vifo hivyo bendera ya Umoja wa Mataifa inapepea nusu mlingoti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad