Wanafunzi watatu wa kike nchini Burundi wametupwa jela kwa kosa la kuichafua picha ya Rais Pierre Nkurunziza.
Image result for rais wa burundi nkurunziza
Kwa mujibu wa Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu, limeeleza kuwa mamlaka za usalama nchini humo ziliwakamata wanafunzi 3 ambao wapo chini ya miaka 18 kwa madai kuwa wamemtukana na kumdhihaki Rais Pierre Nkurunziza.
Shirika hilo limesema kuwa Wanafunzi wote watatu, waliswekwa rumande wikiendi ya wiki iliyopita na Jumatatu hii wamehukumiwa miaka 5 jela kwa makosa ya kumtukana na kumdhalilisha Rais Nkurunziza.
Shirika hilo la Haki za Binadamu, limeeleza kuwa wanafunzi hao walichora picha za Rais Nkurunziza kwenye madaftari na kuharibu sura yake.
Naye, Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za Binadamu Afrika ya Kati, Lewis Mudge amesema kuwa wazazi wa watoto hao wameshangazwa na hatua hizo.
Shirika hilo limekosoa hatua hiyo na kuitaka Serikali kujikita zaidi katika kupambana na watu wanaovunja haki za binadamu badala ya kuwabana watoto wanaoharibu picha za Rais Nkurunziza.
Hii sio mara ya kwanza kwa wanafunzi kukutwa na skendo hiyo, kwani mwaka 2016, vyombo vya dola nchini humo viliwakamata wanafunzi 8 wa sekondari kwa tuhuma za kumkashfu Rais baada ya kumchora Rais Nkurunziza kama kikaragosi.
Wanafunzi watatu wa Sekondari watupwa jela miaka mitano kwa kuiharibu picha ya Rais Nkurunziza
0
March 24, 2019
Tags