Ofisi ya Idara ya Habari Maelezo, imesema kwamba, taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwepo Whatsapp kuhusu kampuni ya mikopo iliyosajiliwa kwa jina la Waziri Mkuu, 'Kassim Majaliwa Foundation' haihusiki na kiongozi huyo.
Taarifa hiyo iliyotolewa siku ya leo imesema kwamba ujumbe huo umekuwa ukiwataka wajasiriamali watume pesa ili waweze kupatiwa pesa ndani ya saa 24.
Wananchi wameaswa kupuuza ujumbe huo huku hatua kali za kisheria zikiwa zinachukuliwa kwa wahalifu hao wanachafua jina la Waziri Mkuu.
Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kwamba, Waziri Mkuu hamiliki, hausiki wala hajasijili kampuni ya aina hiyo ya utoaji mikopo.