Watu 70 Hufariki Kila Siku kwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu

Watu 70 Hufariki Kila Siku kwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema katika kila Watanzania 100,000 Watanzania 269 wanahisiwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu, huku watu 70 wanafariki kila siku kutokana ugonjwa wa Kifua Kikuu ambapo ni sawa na watu watatu hufariki kila saa.

Amebainisha hayo hapo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kifua Kikuu na kutoa tamko kuhusiana na ugonjwa huo katika Hospitali ya Mbagala Jijini Dar es salaam.

Waziri Ummy amesema takribani wagonjwa 154,000 wanaokadiriwa kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu wanapaswa kufikiwa na kuingizwa katika mpango wa matibabu kila mwaka ili kuutokomeza ugonjwa huu nchini.

Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 Duniani zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa Kifua Kikuu, inakadiriwa kuwa wapo wagonjwa takribani 154,000 ambao huugua ugonjwa wa kifua Kikuu kila mwaka.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Mgonjwa wa Kifua Kikuu ambae hajaanza matibabu anaweza kuambkiza Kati ya watu kumi hadi watu 20 kwa mwaka, hivyo jitihada za makusudi zinatakiwa kuendelea kuchukuliwa ili kutokomeza ugonjwa huu nchini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad