Watu Wawili Waliojifanya Raia wa Tanzania Wakamatwa

Watu Wawili Waliojifanya Raia wa Tanzania Wakamatwa
Idara ya uhamiaji Mkoani Kagera imewakamata Tumaini Fransic na Peace Fransic raia wa nchi jirani ya Rwanda waliokuwa wanaishi hapa nchini kinyume cha sheria na kujifanya wWtanzania ambapo wameweza kupata elimu ya msingi, sekondari na chuo kikuu na kujipatia vyeti vya uraia kwa njia ya udanganyifu.

Mrakibu msaidizi wa Uhamiaji,  Butenye Pendo amesema kuwa raia hao walizaliwa hapa nchini baada ya mzazi wao mmoja kuishi nchini kisheria ambaye ni mama yao mzazi lakini baada ya kumaliza elimu ya msingi na kujiunga na sekondari waliweza kutafta vyeti vya uraia ambapo mwenyekiti wa kijiji kyagati bw, Joseph Enerco Kanyonyi na wanawake walili Frida Samweli Kagemulo na Beatrice John Rweyemamu kujifanya wazazi wa watoto hao ili waweze kupata vitambulisho vya uraia na kuweza kupata mikopo ya elimu ya juu.

Afisa Pendo amesema kuwa Frida Samweli Kagemulo alisimama kama mama mzazi wa Tumaini Fransic na Beatrice John Rweyemamu kusimama kama mama mzazi wa Peace Fransic na mwenyekiti kuwasainia ili waweze kupata mikopo ya elimu ya juu kitendo ambacho kilifanikiwa huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Amesema kuwa sheria ya uraia namba 357 iliyofanyiwa marekebisho yake mwaka 2002 inaelezea aina za uraia ulipo hapa nchini kuwa ni; Uraia wa kurithi, Uraia wa kuzaliwa na uraia wa kuandikishwa ambapo mtu anaomba uraia wa kuishi hapa nchini kwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria.

Bw, Pendo amesema kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani na kujibu tuhuma zinazowakabili huku akiwataka wananchi kuacha tabia za kuficha watu wasio wajua kwani wanaweza kujikuta wanakaribisha waharifu na majambazi ambao badae wanaweza kuvuruga amani waliyo nayo katika maeneo yao hasa watu wanaoishi mipakani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad