Watumishi Wadakwa kwa Tuhuma za Kuiba Dawa za Binadamu Ambazoo ni Mali ya Serikali

Watumishi wadakwa kwa tuhuma za kuiba dawa
Jeshi la Polisi Wilayani Chato mkoani Geita linawashikilia watumishi watatu wa idara ya afya mkoani humo kwa tuhuma za wizi wa dawa za aina mbalimbali zinazodaiwa kuwa ni mali ya Serikali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akizungumza na waandishi wa habari jana Machi 12, amesema kati ya watumishi wapo waganga wafawidhi wawili pamoja na mtunza stoo.

Kamanda Mwabulambo alisema watumishi hao wamekamatwa kufuatia operesheni iliyofanywa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo na kupata taarifa zilizowezesha kukamatwa kwa watumishi hao.

Alitaja dawa zilizokamatwa kuwa ni dawa za malaria aina ya Alu pakti 1080, mipira ya kuvaa mkononi box 10 zinazokaa 50 kwenye kila pakiti.

Pia watumishi hao wamekamatwa na vipimo vya malaria box 36, dawa za uzazi wa mpango 41, Alu za watoto paketi 2,292 pamoja na vipimo vya wingi wa damu.

Mkuu wa wilaya ya Chato, Msafiri Mtemi alisema kwamba  kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi kukosa dawa vituoni lakini waganga wafawidhi wamekuwa wakidai dawa zipo na ndipo kamati ya ulinzi iliamua kufanya uchunguzi na kubaini wizi huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad