Waziri Ataka Msanii Huyu kurudi darasani

Waziri Ataka Msanii Huyu kurudi darasani
Waziri wa nchi wa Vijana na watoto nchini Uganda, Bi. Florence Nakiwala, amemtaka mtoto Patrick Ssenyonjo ambaye ni mwanamuziki, kuacha kufanya kazi hiyo na kurudi shule.

Waziri Nakiwala ametoa agizo hilo akiwa kwenye kipindi kimoja cha runinga ya NBS nchini humo, na kusema kwamba mtoto huyo anayejulikana kwa jina maarufu la 'Fresh Kid' kubaki darasani na kusoma, kama wanavyofanya watoto wa umri wake.

Fresh Kid mwenye umri wa miaka 7, amekuwa akikosa vipindi darasani  kutokana na kuwa busy na kufanya matamasha, jambo ambalo limeelezwa ni kukiuka kwa haki zake, na mpaka sasa mtoto huyo tayari ana nyimbo 3 na video moja, huku akifanya matamasha mbali mbali.

Pia Waziri huyo amemtaka meneja wake kuacha kumtumia kuingiza pesa, kwani sheria ya nchi hiyo, hairuhusu ajira kwa watoto.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa Uganda wameonekana kuwa na mtazamo tofauti na Waziri huyo anayeshughulikia masuala ya watoto, wakisema wamuache afanye kitu kitakachomsaidia maishani, kwani wapo watu wazima waliosoma na mpaka sasa hawana ajira.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad