Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amelitaka Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ili kuendelea kuboresha masuala ya Lishe katika jamii.
Ameyasema hayo wakati wa kikao na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid cha kujadili masuala mabalimbali yanayohusiana na Lishe sambamba na miradi inayofadhiliwa na fedha za Umoja wa Ulaya kupitia Shirika la chakula Dunia.
Jafo amewashukuru kwa ushirikiano wanaoutoa katika miradi mbalimbali ya Lishe na hakika wamekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha Lishe Tanzania kwa kuwa Lishe ni suala endelevu na mtambuka.
"Hatuwezi kufikia Taifa la Uchumi wa Kati endapo watu wetu hawatakuwa na lishe bora, ili watu wafanye kazi kwa bidii, waweze kuzalisha na kulipa kodi inavyotakiwa ni lazima wawe na Afya bora wakati wote hivyo kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha lishe bora ni vitu muhimu sana katika kufikia lengo la Kitaifa,”Amesema.
Waziri Jafo Atoa Neno Shirika la Chakula Duniani (WFP)
0
March 27, 2019
Tags