Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefika kuhani msiba wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Fm Ephram Kibonde nyumbani kwao Mbezi Beach.
"Ephraim Kibonde ni kijana ambaye tumefanya nae kazi vizuri sana, ni muwakilishi mzuri katika sekta ya habari haswa kwenye eneo la utangazaji hili ni pengo kubwa" amesema Kassim Majaliwa
Mtangazaji Ephraim Kibonde alifariki jana na kifo chake kimetokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu ambalo lilianza tangu akiwa mkoani Kagera alipokuwa akishiriki katika maziko ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.