Waziri Ummy Mwalimu: Bima Ya Afya Ndiyo Suluhisho La Uhakika Wa Matibabu

Wananchi wametakiwa kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo alipokuwa ziarani Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro akikagua hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.

“Ni muhimu kwa wananchi kuwa na bima ya afya ili waweze kuwa na uhakika wa kupata matibabu ikiwemo dawa bila ya kikwazo cha fedha” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa matarajio ya wananchi mara baada ya kujiunga na bima ya afya ni kupata huduma bora za afya bila usumbufu huku wakiwa na uhakika wa kupata dawa kwa makundi yote ikihusishwa wale wa Bima ya Afya pamoja na Mfuko wa Bima ya Afya Ngazi ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa.

“Mwananchi yeyote ambaye amekuja na bima ya afya, CHF iliyoboreshwa wanapaswa kupata huduma zote, kumwona daktari bure, vipimo bure, na dawa bure” amesema Waziri Ummy na kuongezea “Bila ya kufanya hivyo hakuna umuhimu wa kuwaambia wananchi kukata bima za afya.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amewataka watoa huduma za afya nchini kutoa huduma bora kwa kuzingatia Mwogozo wa Taifa wa Matibabu na orodha ya dawa muhimu huku akiwataka kutoa huduma bora za matibabu kwa kutoa dawa kulingana na mwogonzo unavyobainisha.

“Badala ya kumwandikia unayoitaka wewe au mgonjwa, tumeweka utaratibu weka dawa ambayo ipo kwa mujibu wa mwongozo” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wananchi wanapata dawa katika vituo vya kutolea huduma kwani kumekuwa na malalamiko hapo zamani wagonjwa wakisema madaktari walikuwa waki waambia dawa hakuna huku ili hali dawa zipo.

“Hatutaki kuona wananchi wanalalamika dawa hakuna na kutuona tunadanganya wakati dawa zipo, na mwongozo unasema wazi kama hakuna dawa A mpe dawa B. Alisikika akisema Waziri Ummy.

Ka upande mwingine Waziri Ummy ameupongeza Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa kuhakikisha dawa zinapatikana kwa ufanisi muda wote na kuwataka mafanikio ambayo wameyapata wahakikishe waharudi chini.

“Serikali itaendela kuhakikisha inaboresha Sekta ya afya ili Taifa liweze kuwa na nguvu kazi yenye afya bora kazi yenu nyinyi ni kuhakikisha mnaendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha dawa zinapatikana muda wote” amesema Waziri Ummy.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Dkt. Halima Mangiri ameishukuru Serikali kwa kuuongeza bajeti ya dawa wilayani humo.

Dkt. Mangiri amesema kuwa bajeti ya dawa imekuwa ikiongezeka maradufu mwaka hadi mwaka huku akitolea mfano wa mwaka 2017/18 hali ya upatikanaji wa dawa ilikuwa ni asilimia 86, huku kwa mwaka 2018/19 hali ya upatikanaji dawa ikiongezeka na kufikia asilimia 96.

“Tunaishukuru Serikali, Kwa kweli hali sasa sii kama zamani, tunapata dawa na hali inaridhisha” alisema Dkt Mangiri

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad