Wimbo wa 'Kwangwaru' wapigwa marufuku kutumika mashuleni Kenya

Wimbo wa 'Kwangwaru' wapigwa marufuku kutumika mashuleni Kenya
Bodi ya Uainishaji wa Filamu ya Kenya (KFCB) kupitia Afisa Mkuu Mtendaji Ezekiel Mutua amesema Bodi hiyo haitaruhusu watoto kuimba wimbo wa Kwangwaru ambao una ujumbe ambayo ni kinyume cha maadili.

Mutua alitaja baadhi ya vipande vya wimbo huo, ukifuatilia katika vipande hivyo utagundua kuwa alimaanisha ni wimbo huo ambao ameupiga marufuku.

Mutua alionya kwamba serikali itapiga marufuku muziki wa nje na maonyesho ambayo yanaendeleza uasherati, kudhoofisha utamaduni, desturi na sheria za Kenya.

"Mashindano na discos hizo zote lazima ziratibiwe kuhakikisha kwamba hasa wa nchi za nje hawatoruhusiwa kuja Kenya na kuharibu maadili, tamaduni na mila yetu. Kwa nini wanapiga nyimbo ambapo zimekatazwa kwenye nchi zao? “Alihoji Mutua.

"Tumetangaza hapa kupitia Maafisa wetu wa Polisi, watu kama Diamond na wasanii wengine hakuna kupiga nyimbo zilizofungiwa kwenye nchi zao kuchezwa hapa, hizi muziki kuimba watoto shuleni wanaimbia mama zao 'inama inama' nao wamama wanapiga picha wanao kama ni kitu cha kushangilia eti 'unataka vya pool table na huku umesimama' hawajui maana ya nyimbo mbovu kama hizo, hizo nyimbo tumepiga marufuku zisiimbwe shuleni," alisisitiza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad