JACQUELINE Wolper ameibuka na kusema kuwa kwa sasa yeye ni bosi mwanamke ‘boss lady’ ndio maana ameshindwa hata kuwachamba wale waliomchamba kuwa hajavaa jezi ya taifa katika mechi ya Taifa Stars iliyofanyika wikiendi iliyopita. Akizungumza na Showbiz Xtra, Wolper ambaye ni mkali wa filamu za Kibongo, alisema ingekuwa zamani angewajibu waliomkosoa mitandaoni kwa kuwachamba, lakini kwa sasa hivi anajua kushika hela hivyo hana muda wa kuchambana na watu wa Instagram.
“Sina muda wa kuchamba mtu, najua ushamba unawasumbua sana watu wengi na ndiyo maana kuliko kubishana nao bora nihesabu hela zangu chumbani, mimi kutokuvaa jezi ya taifa haimanishi kwamba siyo mzalendo,” alisema Wolper.