Yanga yamteua Naibu Waziri Mavunde

Yanga yamteua Naibu Waziri Mavunde
Klabu ya soka ya Yanga imeunda kamati maalumu ya kukusanya michango ya kusaidia timu hiyo, ambapo Mwenyekiti wake ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde.

Yanga imetangaza leo kamati hiyo ambayo kazi yake maalum ni kusimamia kampeni hiyo ya kuchangisha fedha kwaajili ya kusaidia timu hiyo ambayo inaelezwa kutokuwa vizuri kiuchumi katika misimu ya hivi karibuni.

Naibu Waziri Mavunde, atasaidiwa na makamu mwenyekiti, Lucas Mashauri huku katibu akiwa ni Deo Mutta.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa kamati itakuwa na jumla ya wajumbe 24.

Hivi karibuni Yanga iliwateua wabunge Venance Mwamoto  wa Kilolo, Seif Gulamali wa Igunga, Dustan Kitandula wa Mkinga Tanga na Said Mtanda ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Nkasi katika kamati yao ya uchaguzi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad