Yaongoza Kwa Kuwa na Simba Wengi Barani Africa

African Wildlife Foundation imesema Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na Simba wengi na kwa upande wa Tembo inashika nafasi ya tatu barani Afrika

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation, Kaddu Sebunya wakati akizungumzia umuhimu wa uhifadhi wa wanyamapori na uhifadhi wa mazingira kwa nchi za Bara la Afrika

Nchi inayoongoza kwa kuwa na Tembo wengi ni Botswana ikifuatiwa na Zimbabwe

Hata hivyo, Sebunya amesema kwa sasa kuna changamoto ya wanyamapori wengi hasa Simba na Tembo kupungua na sababu yake ni uwepo wa majangiri na uwindaji haramu

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad