Zitto abanwa kusema ukweli, apingana kwa kuhoji

Zitto abanwa kusema ukweli, apingana kwa kuhoji
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini kuwa mkweli katika kutoa takwimu za vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi tofauti na takwimu anazozitoa.

Waziri Ummy amelazimika kumjibu Mbunge huyo baada ya kubandika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti ACT - Wanawake, Chiku Abwao ambaye katika maadhimisho ya siku Wanawake jana alisema kwamba mwaka 2019 idadi ya wanawake wanaofariki kwa uzazi imeongezeka mpaka 11,000 kwa mwaka.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa imeeleza kwamba kipaumbele cha Serikali ya CCM kimekuwa ni kuongeza idadi ya wanawake wanaofariki kwa uzazi badala ya kupunguza jambo ambalo limetafsiriwa kama aibukubwa kwa taifa.

Kupingana na kauli hiyo Waziri Ummy amesema kwamba "Kaka yangu, kwa nini husemi ukweli kuwa Takwimu hizi ni za TDHS 2015/16. Na kwamba survey nyingine itafanyika 2019/20 ambapo sina shaka kabisa kuwa vifo vitokanavyo na uzazi vitakuwa vimepungua kwa zaidi ya asilimia 50! Sema ukweli tafadhali,".

"Si kweli. Narudia tena kusisitiza TDHS ni ya 2015/16, takwimu hizi zilikusanywa 2015. hakuna Utafiti mwingine wa kitaifa uliofanyika na kutoa MMR. Hivyo tusubiri utafiti mwingine wa 2019/20 na hapo ndio mnaweza kusema ni jinsi gani Serikali imefanikiwa ktk kupunguza Vifo hivi" Amesisitiza Waziri Ummy



Pamoja na majibu ya Waziri Zitto amemsisitizia waziri kwamba matokeo ya utafiti ambayo bado haujafanyika si sahihi huku akihoji kama anapigana na tafiti zilipo sasa.

"Vikipungua tutamshukuru sana Mungu. Lakini takwimu za sasa kuwa wanawake 556/100,000 Sawa na wanawake 11,000 kwa Mwaka kufariki unazipinga? Kwamba wanawake 30 wanafariki dunia kila siku sababu ya uzazi unapinga? Matokeo ya survey itakayofanyika sidhani kama ni sahihi kujadili" Amesisitiza Zitto Kabwe .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad