Zitto Kabwe Ampongeza Bondia Mwakinyo kwa Ushindi Wake

Zitto Kabwe Ampongeza Bondia Mwakinyo kwa Ushindi Wake

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amepongeza Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo kwa ushindi alioupata jana.

Usiku wa kuamkia leo bondia huyo akiyenza kuwa maarufu zaidi nchini ameshinda pambano lake dhidi Sergio Gonzalez raia wa Argentina.

"Pongezi nyingi kwa Bondia Mtanzania Mwakinyo kwa ushindi wako. Umetupa faraja na furaha Watanzania. Mungu akupe Neema zaidi na uwapige zaidi," amesema Zitto.

Mwakinyo amemchapa Gonzalez kwa TKO katika raundi ya tano ya pambano hilo lililofanyika jijini Nairobi Nchini Kenya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad