Zitto Kabwe anena kuhusu kesi ya Mbowe na Matiko

Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema ameridhika na uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kutupilia mbali rufaa za DPP dhidi ya uamuzi Jaji Rumanyika kutupilia mbali pingamizi zao.

Mapema leo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wameshinda rufaa ya dhamana yao dhidi DPP katika Mahakama ya Rufani.

"Nimeridhika na uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kutupilia mbali rufaa za DPP dhidi ya uamuzi Jaji Rumanyika kutupilia mbali pingamizi zao. Hata hivyo nimesikitishwa sana na Majaji kutoamua kutumia mamlaka yao kutoa dhamana ilhali kuna ‘precedent’ ya Jaji Luanda kwenye kesi ya Lema."amendika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Utakumbuka Novemba 23, 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana. Wawili hao walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Kisutu kufuta dhamana yao ambapo rufani yao ilipangwa kwa Jaji Sam Rumanyika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad