Zitto Kabwe azungumzia nguo ya Rais Magufuli

Zitto Kabwe azungumzia nguo ya Rais Magufuli
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amefunguka kuwa ushindi wa Taifa stars jana dhidi ya timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' umeliunganisha taifa pasi na kujali itikadi za vyama.

Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa, ''mpira umeleta muunganiko kwa taifa na kuleta furaha nchini, huku akifurahishwa na shati alilokuwa amevaa Rais Magufuli lenye rangi ya zambarau ambayo ni rangi  inayotumiwa na chama chake.

"Nguvu ya mpira kuunganisha nchi ni ya aina yake. Kina Samatta kuwezesha Tanzania kufuzu ‘Mataifa Huru Afrika’ #AFCON nchi iliyokuwa imenuna, imejawa furaha. Hata Rais kuonyesha Umoja alivaa shati la Zambarau, rangi ya Chama Cha ACT-Wazalendo akitazama mechi Ikulu", ameandika Zitto.

Taifa Stars imeungana na timu ya taifa ya Uganda, Kenya na Burundi zitakazoiwakilisha Afrika Mashariki katika michuano ya AFCON itakayofanyika kuanzia mwezi June hadi Julai, 2019 nchini Misri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad