ACT Wazalendo Waitisha Maandamano ya Upinzani Nchi Nzima
0
April 06, 2019
Umoja wa Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo umekiri kuwaandikia barua ngome za vijana za vyama vya upinzani nchini kwa ajili ya kushiriki maandamano ya pamoja kupinga uamuzi wa Bunge wa kutofanya kazi na CAG.
Ngome ya vijana ya ACT imesema kuwa inapinga hatua hiyo kwa nguvu zote kwa sababu linakwenda kuua misingi ya ya utawala bora na uwajibikaji.
Pia imesema nia yao ni kufanya maandamano ya amani kwa lengo la kuwakumbusha wabunge na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Bunge ni mali ya umma.
April 2, 2019, Bunge la Tanzania liliazimia kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG, Prof Mussa Assad kwa kutoa kauli yake katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa nchini Marekani ambayo iliyoashiria kulidhalilisha Bunge baada ya kusema kuwa Bunge ni 'dhaifu'.
Tags