Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja [Jina linahifadhiwa] kwa tuhuma za mauaji ya mtoto aitwaye JUNIOR BAKARI @ SIAME [12] Mwanafunzi Shule ya Msingi Hayanga Darasa la III na Mkazi wa Hayanga.
Marehemu alitoweka nyumbani kwao tangu tarehe 09.04.2019 saa 16:00 jioni wakati anatoka masomo ya ziada na ndipo mtuhumiwa hayo alimteka na kuondoka naye kusikojulikana na baadae mtuhumiwa alipiga simu kwa baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye BAKARI SIAME akihitaji kupatiwe fedha Milioni Kumi [Tshs.10,000,000/=] ili aweze kumuachia mtoto huyo ila alimnyonga shingo na kumuua na kukimbilia Mkoa wa Iringa maeneo ya Ipogolo ambapo kikosi kazi cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kilifika na kumkamata na kuja nae Mbeya hadi eneo la tukio.
Ambapo tarehe 13.04.2019 saa 23:00 usiku huko Mtaa wa Shinya, Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jijini na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa [Jina linahifadhiwa] aliwapeleka Askari hadi eneo la tukio alipomnyongea mtoto JUNIOR BAKARI @ SIAME [12] ambapo mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye shamba la mahindi lililopo maeneo ya Mlima Nyoka.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu. Upelelezi unaendelea.
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
Mnamo tarehe 14.04.2019 saa 20:30 usiku huko maeneo ya Ituta, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Barabara kuu ya Mbeya – Tunduma, Jiji la Mbeya. Gari yenye namba za usajili T.775 BYV aina ya Toyota Station Wagon ikiendeshwa na dereva MWAMZI TILA [28] Mkazi wa Uyole ilimgonga mtembea kwa miguu ambaye ni askari G.1008 D/C ANANIA JAMES KIWANGA [36] askari idara ya Upelelezi, Wilaya ya Mbeya mkazi wa FFU Mbeya aliyekuwa kazini kizuizi cha magari Ituta – Iwambi na kumsababishia kifo.
Mtuhumiwa amekamatwa na gari lipo kituoni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Chanzo cha ajali ni mwendokasi. Upelelezi unaendelea.
Aliemteka Mtoto na Kumnyonga Mbeya Amekamatwa na Jeshi la Polisi
0
April 15, 2019
Tags