Wezi wamevunja kituo cha polisi cha Kamorwon kilichopo kaunti ya Nandi nchini Kenya, na kuiba baadhi ya silaha zilikuwepo katika kituo hicho.
Ripoti za polisi zinaonesha kuwa, watu wasiojulikana waliingia katika kituo hicho siku ya Jumanne, Aprili 16, wakati maafisa wa polisi waliokuwa wameshika doria waliondoka na kwenda kutazama mechi eneo jirani na kituo hicho
Waliporejea baadaye usiku, maafisa hao walipigwa na butwa baada ya kugundua kuwa chumba kilichotumika kuhifadhi silaha hizo kimevunjwa huku bunduki tatu na risasi 20 zikiwa hazionekani. Silaha hizo zilikuwa zimefungwa ndani ya gazeti.
"Maafisa wote wa polisi walikuwa wameondoka kutazama mechi ya UEFA katika kituo cha kibiashara na waliporudi usiku, waligundua kuwa ofisi iliyotumika kuhifadhi silaha imevunjwa. Isitoshe bunduki 3 na risasi 20 zilikuwa zimeibwa," ripoti ya polisi ilisema.
Hata hivyo, magazeti mengine yaliyokuwa na risasi 17 na 20 yalikuwa hayajaguswa kulinga na ripoti zaidi za polisi wa kituo hicho.
Mamlaka ya usalama ikiongozwa na kamanda wa polisi wa kituo cha polisi cha Nandi kusini walizuru eneo la kisa hicho na kuwahamasisha maafisa wa polisi kuchukua hatua haraka iwezekanavyo.
Kwa sasa msako dhidi ya wahalifu hao unafanywa ili kuzuia uhalifu ambao huenda ukatekelezwa kwa kutumia silaha hizo.
Askari Polisi Waenda Kuangalia Mpira na Kuacha Kituo Bila Ulinzi.....Wezi Wavamia na Kuiba Bunduki 3 na Risasi 20
0
April 18, 2019
Tags