Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linatarajia kuanza safari za kwenda Afrika Kusini, ambapo safari ya kwanza kweda Johannesburg itakuwa Julai 2019.
Hii itakuwa safari ya tano ya kimataifa kuzinduliwa na ATCL ndani ya miaka 3, baada ya Harare, Lusaka, Entebbe na Bujumbura.
Utakumbuka hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ATCL inatarajia kuanza safari za ndege ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam mpaka kwenye jiji la Guangzhou nchini China ili kuchochea biashara na utalii kati ya Tanzania na China.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ofisi ndogo za ubalozi wa China jijini Dodoma Waziri Kabudi alisema Guangzhou ndio kitovu cha biashara baina ya nchi hizi mbili na safari hizo zinatarajiwa kuana kati ya mwezi June na Septemba ambapo pia mwaka ujao wa fedha Tanzania itafungua ubalozi mdogo kwenye jiji hilo.