Biashara United ni Kisiki, Simba Yategwa Mara

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Biashara United na Simba, rekodi za Biashara United zimeitishia Simba kuelekea mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Karume mjini Musoma.

Katika mechi 10 za mwisho za nyumbani za Biashara United, timu hiyo imefanikiwa kuondoka na ushindi katika mechi sita na kutoka sare katika michezo minne na ikiwa haijapoteza mechi yoyote.

Pia Biashara United inaifukuzia Simba katika kukusanya pointi kwenye michezo yake mitano iliyopita, Simba ikiwa imekusanya jumla ya pointi 12 ikifuatiwa na Biashara United ambayo imekusanya pointi 11.

Kikosi cha Simba katika mchezo huo utakaopigwa saa 10:00 jioni ni:

1. Aishi Manula, 2. Nicholas Gyan, 3. Asante Kwasi, 4. Paul Bukaba, 5. Juuko Murdhid, 6. Said Ndemla, 7. Haruna Niyonzima, 8. Mzamiru Yassin, 9. John Bocco, 10. Meddie Kagere, 11. Mohamed Ibrahim.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad