Bobi Wine Aandaa Maandamano Uganda

Bobi Wine aandaa maandamano Uganda
Msanii na mbunge, Bobi Wine anatarajia kuwasilisha rasmi barua Polisi kuwafahamisha kuhusu maandamano yake ya amani kupinga kuzuiwa  vyanzo vyake vya mapato.

Hatua ya Bobi Wine inafuatia polisi kuzuia tamasha lake kwa madai kwamba hawakuwa na uwezo kudhibiti maelfu ya mashabiki wake.

Jana Bobi Wine ambaye ni mbunge wa upinzani, alitiwa nguvuni kwa saa kadhaa baada ya kumkamata alipokuwa njiani kuelekea kwenye hoteli iliyoko iliyopo Ziwa Victoria ambako alikuwa akipanga kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu  hatua ya Serikali kumzuia kufanya tamasha lake la Pasaka.

Rais Museveni anasema hatavumilia matamasha yanayochanganywa na siasa. Wine alisema Museveni anataka kuwazuia wanamuziki wote ambao hawamuungi mkono.

''Rais Museveni amewaagiza polisi kuzuia matamasha yangu kwa sababu hapendi kusikia ninachokiimba. Alitaka mimi niwe kama baadhi ya wasanii wanaoimba nyimbo za kumsifu na nilipokataa akaamua kuwa hataniruhusu kufanya onyesho lolote la muziki wangu nchini Uganda,’’ alisema.

Video ya kukamatwa kwake ilionyesha polisi wa kuabiliana na ghasia wakiingia kwa nguvu ndani ya gari lakekatika eneo la Busabala.

Bobi Wine alikamatwa na kuingizwa katika gari la polisi na kupelekwa eneo lisilojulikana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad