Bobi Wine kurudishwa rumande,mashirika ya haki za binadamu yalia na Serikali ya Uganda

Kumekuwa na hisia kali kufuatia taarifa kwamba mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amerudishwa rumande mpaka Mei 2 siku ya Alhamisi wiki hii. Ameshtakiwa kwa kushiriki katika maandamano ya ‘haramu’ mnamo mwaka jana ya kupinga kodi ya kutumia mitandao ya kijamii maarufu Uganda kama OTT.



Alionekana akitembea huku akiwa amefungwa pingu mikononi kabla ya kuabiri basi la magereza kuelekea katika gereza kuu la Luzira mjini Kampala.

Haya yanafanyika siku chache baada ya kuwa katika kifungo cha nyumbani.

Ameshtakiwa kwa kuandaa maandamano ya umma kinyume na sheria, na alizuiwa siku ya Jumatatu katika kituo cha polisi cha Naggalama kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Kwa mujibu wa BBC.  Msemaji wa idara hiyo Fred Enanga amesema Bobi Wine aliongoza maandamano hayo mwaka jana pasi kwanza kuomba ruhusa kutoka kwa polisi.

“Anazuiwa na polisi na uchunguzi unaendelea,” ameliamba shirika la habari la AFP.

Kampeni mpya imeanzishwa katika mitandao ya kutaka Bobi Wine aachiliwe huru huku baadhi wakizungumzia hatua hiyo kama ya kutia wasiwasi.

Ujumbe wa Twitter wa @CossyWyne: Fighting for equal rights and justice #FreeBobiWine Hakimiliki ya Picha @CossyWyne@COSSYWYNE
Ujumbe wa Twitter wa @kaysafi1: May we learn to be as strong &resilient as you've been so far Bobi Wine. May we speak on the things that matter &emulate you.You make not only I but many like myself proud of being youths. You give us purpose. We love you! Stay strong. #FreeBobiwine ✊🏾✊🏾 Hakimiliki ya Picha @kaysafi1@KAYSAFI1
Mashirika ya kutetea haki za binaadamu likiwemo la Marekani, Tom Lantos Human Rights Commission, na shirika linaloshinikiza uongozi wenye maadili na demokrasia kwa wote – Vanguard Africa, yameshutumu hatua hiyo ya serikali ya Uganda.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, mashirika hayo yametaka serikali iheshimu uhuru wa kujieleza na kushinikiza kuachiwa kwa mwansiasa huyo wa upinzani.

Aliyekuwa waziri mkuu wa New Zealand Helen Clark amejiunga katika kutoa ujumbe huo wa kutaka Bobi Wine aachiwe kwa kuitisha mshikamano wa kitaifa katika kulinda maisha na afya ya mwanasiasa huyo wa Uganda.

Ujumbe wa Twitter wa @HelenClarkNZ: Very distressing to see #Uganda 🇺🇬 opposition MP & popular musician #BobiWine detained again. Last year in detention he was beaten & tortured. International solidarity is vital to protect Bobi's health & life #FreeBobiWine @commonwealthsec @VanguardAfrica Hakimiliki ya Picha @HelenClarkNZ@HELENCLARKNZ
Bobi Wine aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani katika kile ambacho polisi walisema ilikwa ni hatua ya kumzuwia mwanasiasa huyo wa upinzani kufanya mikutano iliyo kinyume cha sheria.

“Hizo zilikuwa ni hatua zilizochukuliwa chini ya sera ya kuzuwia ili kulinda sheria na utulivu wa umma. Wakati bado anatishia kufanya mikutano kinyume cha sheria ,maafisa wetu wa ujasusi watatusaidia kumpata na tutaweza kuona ni nini kitakachofuatia. Hata hivyo hadi sasa tutaendelea pale majeshi yetu kwasababu hili limekuwa ni suala la usalama wa taifa ,” amesema Msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga.

Saa kadhaa awali , Bobi Wine alikuwa ametangaza mpango wa kufanya maandamano ya umma kote nchini kupinga hatua ya polisi kuendelea kuweka vikwazo dhidi ya tamasha zake za mziki na ukatili dhidi ya wanasiasa wa upinzani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad