Bunge lakanusha Spika kumshinikiza CAG Ajiuzulu

Bunge lakanusha Spika kumshinikiza CAG AjiuzuluOfisi ya Bunge Tanzania imekanusha taarifa ya kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuandikia barua Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG akimtaka kujiuzulu au kujieleza kwa mwajiri wake.


Kupitia taarifa maalum iliyowasilishwa kutoka kitengo cha mawasiliano ya Bunge, imesema kuwa barua hiyo hawaitambui na si ujumbe wa Spika Job Ndugai kwenda kwa CAG, Prof. Assad.

Taarifa hiyo imesema kuwa, "kumekuwepo kwa taarifa nyingi za uzushi kupitia mitandao ya kijamii, tangu Spika Job Ndugai azungumze na waandishi wa habari, moja wapo ni barua ya yenye kichwa cha habari "wito wa ama kujiuzulu au kujieleza kwanini usiadhibiwe na mwajiri wako". Tunatahadharisha umma barua hiyo ni ya uzushi hivyo ipuuzwe, ofisi ya Spika na ofisi ya Bunge haihusiki kwa namna yeyote na barua hiyo".

Hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari Spika Ndugai alimtaka Prof. Assad kujieleza kwa Rais au kujiuzulu nafasi yake.

"Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi  ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au la! maana tushamwambia  hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais", alisema Spika Ndugai.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad