Bunge Lapitisha Azimio la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Kamati ya Maadili imemtia hatiani kwa kulidhalilisha Bunge,Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali CAG,Prof.Mussa Assad,kwa kusema kuwa "Bunge ni dhaifu".

Kufuatia hatua hiyo Kamati imetoa mapendekezo ya Bunge kutofanya kazi na CAG,Prof.Asaad.

Akisoma ripoti ya kamati hiyo bungeni leo Aprili 2 mwaka 2019, mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka amesema kamati yake imemtia hatia kwa kuvunja kifungu cha 26 E cha Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.

Amesema Profesa Assad wakati wa mahojiano na kamati hiyo alionyesha dharau na hakuonyesha kujutia maneno yake

 "Prof. Assad alikiri mbele ya kamati kuliita Bunge dhaifu lakini alipingana na tafsiri ya neno 'dhaifu' iliyopo kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu inayosema 'goigoi, hafifu, isiyo imara' akisitiza kiuhasibu udhaifu ni 'upungufu'.

"Tuliangalia maana ya neno upungufu kwenye kamusi tukabaini ni 'isiyo kamili, isiyo imara', hivyo alidhamiria kulidhalilisha Bunge.

 "Tulimuuliza CAG Assad kama ataacha kulitumia neno udhaifu akasisitiza ataendelea kulitumia na hakujutia kulitumia dhidi ya Bunge.CAG hakuomba msamaha wala kujutia na akasisitiza ataendelea kulitumia neno hilo".Amesema Mwakasaka

Baada ya ripoti hiyo ya kamati, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alitoa nafasi kwa wabunge kujadili jambo hilo huku wabunge wakipishana maoni yao,   kukubaliana na uamuzi huo na wengine kupinga .

Baada ya wabunge kutoa maoni yao,  Dk Tulia amelihoji Bunge kuhusu hoja hiyo, akiwakata wanaokubaliana na jambo hilo kusema ndio na wasiokubaliana na suala hilo kusema sio,  "waliosema ndio wameshinda. "

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad