CAG azibana CHADEMA, CCM kwenye ripoti


Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad, katika ukaguzi uliofanyika katika vyama vya siasa, CCM ilibainika kuwa haijawasilisha makato ya wafanyakazi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mukhtasari wa kile kilichomo kwenye ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2017/18, CAG amesema kwamba kiasi cha fedha cha shilingi bilioni 3.74 za wanachama wake.

Mbali na Chama Cha Mapinduzi, CAG ameeleza kwamba, "Tumebaini CHADEMA ilinunua gari jipya aina ya 'Nisan Patrol' kwa Sh milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini.

Ameongeza kwamba gari hilo kwenye taarifa ya fedha ilioneshwa kwamba kama mkopo kwa mwanachama huyo bila kuwa na makubaliano ya mkopo yaliyosainiwa kati ya mwanachama huyo na bodi ya wadhamini wa CHADEMA.

Mbali na CHADEMA, CAG amesema kwamba pia wamebaini kuwa majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya Bodi ya Wadhamini.

Mbali n ripoti ya vyama, CAG amesema katika ukaguzi wamebaini kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilinunua mashine za BVR 8000 kwa ajili ya usajili wa wapiga kura, mashine 5000 hazikukidhi vigezo na hivyo kutolandana kimatumizi na zile zilizonunuliwa awali na NIDA na RITA na  kusababisha hasara ya Sh862.08m.

Hata hivyo ukaguzi wa CAG umebaini kwamba katika ukaguzi maalumu uliofanywa katika ununuzi wa sare za askari polisi uliofanywa na Jeshi la Polisi nchini, na kwamba walibaini kwamba jeshi lililipa Sh16.66 bn bila kuwepo kwa ushahidi wa uagizaji wala upokeaji wa sare hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad