CCM Yatoa Tamko Kuhusu Katiba Mpya

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally amesema kwa sasa hawezi kutoa neno lolote kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya kwa kile alichokisema neno lake litapelekea kulifanya suala hilo lisijadiliwe tena hasa na Wabunge wa CCM, ikiwa siku chache baada ya Bungeni jijini Dodoma kuibuka kwa suala

la Katiba mpya baina ya Wabunge wa Upinzani na CCM, wakati wa kujadili suala Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Akizungumzia suala la Katiba mpya Katibu Mkuu huyo wa CCM amesema yeye alifuatilia hoja za Wabunge wa Upinzani ambao walitoa michango yao wakati Bunge lilipokaa kama Kamati kujadili bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ambapo amesema Katiba mpya ni sehemu mambo yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi wa chama hicho.

“Nilikuwa nafuatilia kwa karibu mijadala inayoendelea bungeni na hasa kuhusu Katiba mpya, malumbano bila kutukanana ndiyo afya ya demokrasia, sitajibu suala hilo kwa sasa kwa sababu nikitoa kauli yangu nitaufunga mjadala huo.” amesema Bashiru

Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadiro ya mapato na matumizi ya Wizara zao kwa mwaka 2019/2020.

Wiki iliyopata Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Muungano na Mazingira, Katiba na Sheria pamoja na Wizara ya TAMISEMI zote ziliwasilisha makadirio yao ya bajeti kwa mwaka ujao wa fedha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad