Chuchu na Aunt Wapewe Tuzo za Kutendwa

Chuchu na Aunt Wapewe Tuzo za Kutendwa
ANASEMAJE? Mwanamama anayefanya poa kunako Bongo Muvi, Chuchu Hans amesema yeye na mwigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel wanastahili tuzo kutokana na maumivu ya kuumizwa na wenza wao.

Chuchu aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, mara nyingi wao ndiyo wamekuwa watu wakuumizwa na wapenzi wao au baba wa watoto wao, jambo ambalo linawauma mno.

“Mimi na Aunt naona tunastahili kupewa tuzo kwa kuwa tumeumizwa sana hadi sasa mtu unakata tamaa ya kuingia kwenye uhusiano kabisa,” alisema Chuchu ambaye hivi karibu mzazi mwenzake, mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ alidaiwa kutoka kimapenzi na mwanamke mwingine kama ilivyotokea kwa mzazi mwenza wa Aunt, Moze Iyobo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad