DC Jokate avuna mamilioni Kisarawe ndani ya miezi 6

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo amefanikiwa kuvuna mamilioni ya fedha kwenye kampeni yake ya ‘Tokomeza Zero’ yenye lengo la kuchangia elimu wilayani humo.

DC Jokate miezi mitatu iliyopita alianzisha harambee ya kuchangia elimu kupitia kampeni hiyo ya Tokomeza Zero, ambapo alianzia kampeni wilayani humo na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Tsh milioni 125.

Kwenye kampeni hiyo aliyoanzisha ikiwa ni miezi 6 tu iliyopita, DC Jokate ameonekana kuungwa mkono na viongozi mbalimbali Serikalini, Taasisi, Mashirika na wadau mbalimbali wa elimu.

Kwenye harambee hiyo ya kwanza iliyofanyika Septemba 27 mwaka jana, Jokate alishukuru kwa kusema “Kutokana Na Maombolezo Ya Msiba Ukerewe, Serikali ya Wilaya ya Kisarawe kwa pamoja tuliamua kuhairisha shamrashamra za programu yetu ya Tokomeza Zero Harambee Pale Minaki Sekondari, tukasimama na kuombea ndugu zetu waliopoteza maisha lakini pia kutoa faraja kwa kuchangia Milioni Moja kama rambirambi kutoka Wilaya ya Kisarawe. Lakini tuliruhusu waliofika kuchangia na baada ya kupiga mahesabu leo tumeweza kuchangisha Milioni 125.062 katika awamu hii ya kwanza. Hii ahadi ya michango ya pesa taslimu imevuka lengo letu la awali ambalo lililuwa ni Milioni 100 ilituweze kuhudumia makambi ya wanafunzi mpaka mwezi wa kumi na moja ambapo wataanza mitihani yao ya mwisho ya taifa. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wananchi wenyeji wa Kisarawe kwa kuitikia wito kwa wingi sana ila pia na wadau wetu kutoka nje ya Kisarawe. Tunawashukuru sana. Mungu awaongezee pale mlipopunguza.“.

Kampeni hiyo ya Tokomeza, ilianza kupata umaarufu kwenye mitandaoni ambapo watu wengi maarufu wakaanza kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kampeni hiyo, haikuishia hapo tu Jokate akaipanga kwa ukubwa ambapo ambapo awamu hii aliifanyia katika Ukumbi wa Mlimani City wikiendi ilyopita ya Machi 31, 2019.

Kwenye harambee hiYO, Jokate alifanikiwa kwa kiasi chake kwani ilihudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo viongozi wakuu serikali.

Kwa makadirio madogo ya michango iliyokusanywa wakati wa harambee hiyo ikioneshwa live, ilikuwa ni zaidi ya Tsh milioni 149, huku wengine wakiahidi kujenga madarasa, kutoa msaada wa vitabu, n.k .

Hata hivyo DC Jokate ameahidi kutoa taarifa rasmi ya makusanyo yote ya harambee hiyo, mapema atakapomaliza mahesabu.

Kampeni ya Tokomeza Zero ilianzishwa na DC Jokate miezi takribani 6 ikiwa ni miezi mitatu tangu ateuliwe na Rais Magufuli mnamo July 28, 2018.

Hata hivyo, Jokate bado anahitaji misaada zaidi kwa watu watakaoguswa na kampeni yake ya Tokomeza Zero’ .

UNAWEZA UKACHANGIA KWA KUPIGA NAMBA 0677062070 JINA LITATOKEA TOKOMEZA ZIRO KISARAWE.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad