Amiri Kilangalila.
Diwani wa Machame Magharibi Martin Munisi ameungana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuwajibishwa kwa yeyote atakayeweza kudharau chombo hicho.
Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari hii leo Munisi amesema
"Kuhusu CAG . Taarifa ya CAG ni nzuri sana na inalenga kuzitetea pesa za wanyonge wa nchi hii lakini maneno ya kuudhi aliyoyatumia kulitusi bunge letu huwezi ya husisha na taarifaa maana kwenye taarifa hakuna mahali wakaguzi wametumia maneno hayo ya kutukana bunge hayo yametumiwa na mtu mmoja na kama ni kuwajibika awajibike mtu mmoja kwa kauli yake kuwa Bunge ni dhaifu binafsi ninaamini bunge letu siyo dhaifu na nina imani taarifa ya CAG ambayo imejaa mambo mazuri sana kwa nchi yetu iliyofanywa na vijana wazalendo wa nchi hii itafanyiwa kazi na wote walio husika kuhujumu pesa za umma wawekwe kwenye mikono ya sheria "
Aidha ametoa Pongezi kwa halmashauri ya Hai kupata hati safi.
" hii ni kazi nzuri iliyofanywa na madiwani wa CCM chini ya usimamizi mzuri wa Mkuu wa wilaya ambaye ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za Serikali ndani ya wilaya Hai Mkurugenzi ambaye ndiye afisa masurufu na wataalum wote wa Halmashauri ya wilaya Hai wanafanyakazi mzuri sana na wananchi wetu kwa Asilimia kubwa wamekubali kazi mzuri ya utelekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM"alisema Munisi
Katika hatua nyingine diwani huyo amesema kuwa wananchi wa kata hiyo wamekuwa wakiendelea na shughuli zao bila kumuona mbunge wao ambaye ndie mfuatiliaji wa shughuli za maendeleo katika jimbo lao.
"Hai tuna mwaka wa pili hatujawahi Muona mbunge kwenye shughuli yoyote ya Serikali au ya kuwawakilisha wananchi tangu niwe Diwani huu ni mwaka wa pili sijawahi mwona Mbunge wetu Freman Mbowe kama ukitaka kudhibitisha hili nenda kwa Mkurugenzi atakupa daftari la mahudhurio kama ukikuta ndani ya miaka miwili mbunge ameshirikiana nasi katika kikao chochote basi niitwe mwongo Hai kwa Miaka miwili hatujui alipo mbunge na hakuna tamko lolote la kumpongeza lililotoka Hai hizo picha anazosambaza anajiita katibu wa mbunge siyo za Hai yeye ndiye anajua alikozitoa"alisema Diwani.